LOWASSA JE SLAA YUPO NAWE.
      Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa.     Na Waandishi Wetu   N I  kweli, ukweli ni huu! Wakati maelfu ya watu nchini wakiamini  kutoonekana hadharani kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na  Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa kunatokana na kuchukizwa na  kitendo cha kukaribishwa kwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na  kupewa fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho, ukweli wa jambo hilo  umeibuliwa, Uwazi linakupa zaidi.     Edward Lowassa na alipochukua fomu ya kuwania urais kupitia Chadema.   Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, aliyeomba hifadhi ya  jina lake, ameliambia gazeti hili kuwa, madai yanayotolewa na watu  mitaani na katika mitandao ya kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na  kitendo hicho ni ya uongo.     ALIANZA DK. SLAA, MBOWE MH!   Mjumbe huyo alisema kuwa, Dk. Slaa ndiye mtu wa kwanza ndani ya Chadema  kutoa wazo na hatimaye kushiriki kikamilifu katika vikao vya kumwezesha...