Posts

Showing posts from October, 2014

BBC KUPIGWA MARUFUKU NCHINI RWANDA, KURA YA MAONI YAENDELEA

Image
Bunge nchini Rwanda limepiga kura ya kupiga marufuku BBC nchini humo, kufuatia kipindi maalum cha Televisheni kilichoitwa ''Untold story'' kuhusu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 kilichopeperushwa na BBC. Kipindi hicho kilihoji uhusika wa baadhi ya maafisa wakuu serikalini juu ya yale yaliyotokea wakati wa mauaji ya kimbari. Bunge hilo linataka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya BBC kwa kupeperusha kipindi hicho ambacho wanasema kinahujumu mauaji ya Kimbari na pia kukana mauaji dhidi ya watutsi.