Posts

Showing posts from August, 2015

LOWASSA JE SLAA YUPO NAWE.

Image
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa. Na Waandishi Wetu N I kweli, ukweli ni huu! Wakati maelfu ya watu nchini wakiamini kutoonekana hadharani kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa kunatokana na kuchukizwa na kitendo cha kukaribishwa kwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa na kupewa fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho, ukweli wa jambo hilo umeibuliwa, Uwazi linakupa zaidi.  Edward Lowassa na alipochukua fomu ya kuwania urais kupitia Chadema. Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, aliyeomba hifadhi ya jina lake, ameliambia gazeti hili kuwa, madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo. ALIANZA DK. SLAA, MBOWE MH! Mjumbe huyo alisema kuwa, Dk. Slaa ndiye mtu wa kwanza ndani ya Chadema kutoa wazo na hatimaye kushiriki kikamilifu katika vikao vya kumwezesha Lowassa kuji