Posts

Showing posts from November, 2015

SERIKALI YA MAGUFULI JUU YA KULISHWA SUMU MKUU WA JESHI LA WANANCHI JWTZ.

Image
Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Tanzania (DIT), Benedict Ngonyani, anayetuhumiwa kusambaza taarifa katika mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jenerali, Davis Mwamunyange, amelishwa sumu, umewasilisha mahakamani kusudio la kukata rufaa kupinga mshtakiwa huyo kupewa dhamana. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage, ilitengua hati ya kuzuia dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP).     Kabla ya uamuzi huo, hakimu alisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili na alikubaliana na maombi ya utetezi ya kumpa dhamana kwa kuwa sababu za DPP kuzuia dhamana hiyo hazikuwa na msingi wa kisheria.  Wakili wa Serikali Mkuu, Theophil Mutakyawa aliwasilisha kusudio hilo jana saa 7:00 mchana, kwamba upande wa Jamhuri haujaridhika na uamuzi wa m