SERIKALI YA MAGUFULI JUU YA KULISHWA SUMU MKUU WA JESHI LA WANANCHI JWTZ.
 
  Upande  wa Jamhuri katika kesi inayomkabili mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia  Tanzania (DIT), Benedict Ngonyani, anayetuhumiwa kusambaza taarifa  katika mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi  Tanzania (JWTZ), Jenerali, Davis Mwamunyange, amelishwa sumu,  umewasilisha mahakamani kusudio la kukata rufaa kupinga mshtakiwa huyo  kupewa dhamana.     Mwishoni  mwa wiki iliyopita, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es  Salaam, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage,  ilitengua hati ya kuzuia dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo iliyowasilishwa  na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP).     Kabla  ya uamuzi huo, hakimu alisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili  na alikubaliana na maombi ya utetezi ya kumpa dhamana kwa kuwa sababu za  DPP kuzuia dhamana hiyo hazikuwa na msingi wa kisheria.      Wakili  wa Serikali Mkuu, Theophil Mutakyawa aliwasilisha kusudio hilo jana saa  7:00 mchana, kwamba upande wa Jamhuri haujaridhika n...