Tanzania yatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye roho mbaya zaidi AFRIKA.
   
   www.mambobomba.blogspot.cominakuletea taharifa kali ya wiki.   
    
   
   
     
   
    
   
   
   
   
Kwa mujibu wa ripoti ya World Giving Index 2014, Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye watu wenye roho mbaya barani Afrika.
Hiyo
 ni kwa mujibu wa utafiti uliodhaminiwa na Charities Aid Foundation 
(CAF) na kufanywa na kampuni ya utafiti ya Gallup na kuhusisha nchi 135 
duniani kote. Data hizo zilikusanywa kuanzia mwaka 2013.
Tanzania
 ilikamata nafasi ya 14 kati ya nchi 24 zilizofanyiwa utafiti na 
kukamata nafasi ya 87 duniani ikiwa na asilimia 27 nyuma ya Kenya ambayo
 imekamata nafasi ya kwanza Afrika na nafasi ya 15 duniani ikiwa na 
maana kuwa ina watu wakarimu na wanajitolea zaidi kusaidia.
Nchini zenye watu wenye roho mbaya zaidi ni Tunisia, Misri na Congo.
Utafiti huo ulifanywa kwa kuwauliza washiriki kama wamewahi kufanya mambo haya:
  
Wamechanga
 fedha kwenye charity yoyote, wamejitolea kusaidia taasisi yoyote, 
kumsaidia mtu asiyemfahamu au kumsaidia wasiyemfahamu baada ya kumuomba 
msaada.
Marekani imeongoza kwenye orodha hiyo.

 
 
