DIAMOND NA JK IKULU KUNANI!
NYUMA ya ukaribu wa Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, kuna siri nzito kufuatia mambo mbalimbali yanayojitokeza kati yao kila kukicha, jionee picha hapa chini.
KAMA MWANAFAMILIA
“Mara nyingi siku hizi ninapokutana na rais wetu nimekuwa nikijisikia kama mwanafamilia kutokana na jinsi anavyoniongoza na kuthamini kila kazi inayotokana na muziki wangu jambo ambalo ni la kujivunia sana kwenye maisha yangu maana ninaona wasanii kibao katika nchi nyingine hawafanyiwi haya tunayopata sisi wasanii wa Tanzania kutoka kwa mheshimiwa.
“Nina uhuru mwingi sana wa kuzungumza naye na amekuwa akifanya hivyo karibia kwa kila msanii na kutambua hilo na ndiyo maana hata tuzo zangu nilizopata mwaka 2014 nilimjulisha pamoja na yeye kujua na kunipongeza lakini pia mafanikio hayo naamini yamepatikana kutokana na sapoti yake kubwa ambayo amekuwa akinipatia mara kwa mara.
Comments
Post a Comment