RAPING,ASKARI WA KITUO KIKUU SHINYANGA JELA KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA.
Askari
polisi wa kituo kikuu cha Shinyanga aliyefahamika kwa jina moja la
Alex, amewekwa korokoroni akituhumiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha
kwanza , mkazi wa kata ya Ngokolo mjini hapa na kumsababishia maumivu
makali sehemu za siri.
Kamanda
wa polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha, alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo huku akisema jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi ili
kubaini ukweli kamili, akigoma kutaja jina kamili la mtuhumiwa huyo hadi
hapo uchunguzi utakapokamilika.
“Tunaendelea kufanya uchunguzi, lakini sina haja ya kutaja jina lake kwa sasa hadi hapo tutakapothibitisha hilo,” alisema kamanda Kamugisha.
Akizungumza
na mwandishi wetu jana, mama mdogo wa mwanafunzi huyo, Neema Elisha,
alisema tukio hilo lilitokea Januari 4, mwaka huu, saa 8:00 usiku,
wakati binti huyo alipotoka nje kujisaidia na kukutana na polisi huyo
aliyemvutia ndani mwake na kutekeleza unyama wake.
Elisha
alisema aliposhituka muda huo, hakuweza kumuona binti yake kitandani
huku mlango ukiwa wazi na alipomfuatilia hakuweza kumkuta chooni, hivyo
aliporudi kusubiri alimuona anatokea kwa polisi huyo akiwa mnyonge.
“Siku hiyo mume wangu hakuwapo, nililala na binti yangu kitanda kimoja lakini ghafla sikumuona mtoto kitandani, nilipotoka nje kumuangaza sikumuona na baadaye nikamuona anatokea akiwa mnyonge,” alisema Elisha.
Alisema
alipomhoji hakuweza kumwambia hadi alipomtisha ndipo aliposema
alipoenda kujisaidia alivutwa ndani na polisi huyo na kumlazimisha
kufanya naye mapenzi kwa nguvu huku akimtisha na kumziba mdomo.
Hata
hivyo, mwanafunzi huyo alisema askari polisi huyo ambaye ni mpangaji
katika nyumba hiyo anayoishi mama yake mdogo, alikuwa na kawaida ya
kumtongoza kila wakati na kumkatalia, lakini siku hiyo ndipo alipopata
nafasi ya kumbaka.
“Nilisikia
maumivu makali wakati ananiingilia kimwili, kwani wakati anafanya hivyo
alinizidi nguvu huku akiniziba mdomo ili nisiweze kufurukuta,” alisema mwanafunzi huyo.
Comments
Post a Comment