Ramadhani njema, Mh.E Lowassa amewatakia waislam mfungo mwema .
Waislam wapata Salam za Ramadhani kutoka kwa aliyekuwa waziri mkuu Mstaafu mwenye mahamuzi magumu.
Waziri Mkuu wa Mstaafu ambaye pia alikuwa mgombea urais kwa Tiketi ya Chadema ameibuka na kuwatakia mfungo mwema waislam wote nchini.
Kupitia ukurasa wake wa facebook. Lowassa ameandika; "Waumini wa kiislam Tanzania wanaungana na wenzao kote duniani katika kutimiza moja ya nguzo tano Za uislam kufunga Ramadhan.
"Mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ni kipindi muhimu sana kwa waislam kuwa karibu na mola wao.
"Kwa niaba ya Mke wangu Regina na Mimi binafsi, nachukua nafasi hii kuwatakia waislam wote nchini,kila la kheri na baraka tele kwenye mwezi huu.
"Hata hivyo nasononeshwa na hali ya maisha ya watanzania nchini hivi sasa inavyozidi kuwa ngumu.Bei Za bidhaa mbalimbali zimezidi kupanda na zaidi kuadimika kwa sukari ambayo ni bidhaa muhimu sana hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
"Nawaomba wafanyabiashara kupunguza bei ya bidhaa hususan zile muhimu katika mwezi huu, ili ndugu zetu waislam watimize Ibada yao vizuri.
"Aidha kwa waislam nawaomba tutumie mwezi huu kuliombea taifa letu amani,upendo na mshikamano.Lakini zaidi kuomba haki na hamu ya watanzania kuona mabadiliko ya kisiasa yanafanyika kwa amani na wale wenye ulevi wa kuminya haki hiyo, hawapati tena nafasi kutekeleza uovu wao na zaidi Kuwaombea viongozi wetu wawe na hofu ya Mungu.
"Mbarikiwe sana na nawatakia kila la Kheri."
Comments
Post a Comment