Aunt Ezekiel katika harakati za kusaka Mtoto,Dubai
Mwigizaji
nguli katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel (pichani) anadaiwa
kuanza kusaka mtoto ikiwa ni miaka miwili tangu afunge ndoa na Sunday
Dimonte.
Kwa
mujibu wa rafiki wa karibu wa Aunt, siku si nyingi staa huyo atakwenda
kuweka makazi ya muda kwa mumewe Dubai hadi atakapopata ujauzito.
Akizungumza
na Amani hivi karibuni, rafiki huyo ambaye aliomba jina lake
lihifadhiwe kwa kuogopa kusutwa na ‘matarumbeta’, alisema wengi wanadai
mume wa Aunt yuko jela kwa hiyo ili kuwahakikishia kuwa kitu hicho
hakipo ameamua aende kuishi Dubai kwa muda hadi atakaponasa ujauzito.
“Kama
mipango yake itakwenda vizuri, baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani
kupita ataondoka na safari hii atakaa sana Dubai hadi Mungu
atakapomjalia kupata mimba ndipo atarejea Bongo. Lakini baadaye
ataondoka tena kwani hata kujifungua amependa akajifungulie Dubai,” alisema rafiki huyo.
Baada
ya kupata nyepesinyepesi hizo, Amani lilimtafuta Aunt na kufanikiwa
kukutana naye uso kwa uso alipoulizwa alisema hapendi kuweka hadharani
mambo yake na mumewe lakini kuhusiana na ishu ya kwenda kuishi Dubai,
muda si mrefu ataondoka.
“Nadhani
unajua kuwa mke na mume Mungu akiwajalia afya njema ni muhimu ndoa
ijibu kwa kupata mtoto, sasa kuhusu kwenda kuishi Dubai ndiyo mipango
yangu.
“Nataka kuwakomesha wale wanaodai kuwa mume wangu amefungwa! Sitaki kuwajibu kwa maneno, nataka kuwajibu kwa vitendo,” alitamba Aunt.
Chanzo: Amani/Gpl
Chanzo: Amani/Gpl
Tupe maoni yako hapo Chini..!!
Comments
Post a Comment