SUDAN; binti wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kuasi uislamu ndani ya Italia
Binti wa SUDAN aliyehukumiwa kifo kwa kuasi dini ya UISLAMU ahamishiwa ITALIA
Meriam na familia yake wameondoka na ndege ya Serikali ya Italia wakisindikizwa na Makamu Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia, Lapo Pistelli.
Awali Meriam alihukumiwa kifo na viboko 100 baada ya kuasi dini ya baba yake ambaye ni Muislamu na kuolewa na Mkristo, Daniel Wani.
Baadaye mwanamke huyo alifanikiwa kuachiwa huru baada ya wanaharakati kuingilia kati japo alikamatwa tena kabla ya kuachiwa na kukaa katika ubalozi wa Marekani, Khartoum.
Meriam amekana katu katu kuwa mwislamu dhidi ya tuhuma zilizomkabili ingawa anatumia majina yenye asili ya kiislamu lakini yeye hakuwahi kuwa mwislam hata kidogo.
Merian alihamia Italia kwa mkono wa serikali ya Marekani, kama unavyojua serikali ya Marekani haipendi kuingilia masuala yadini hivyo iliamua kumwachia Italia suala la Merian.
Merian anampenda mpenzi wake wala suala la dini siyo kikwazo penzi lameshakamata usikani kwani alishafunga ndoa na anamtoto kama wanavyo onekana katika picha hapo juu.
Comments
Post a Comment