KAHABA WA KITANZANIA MWENYE ROHO NGUMU AJIELEZEA ALIVYOKUWA AKISAMBAZA NGOMA BONGO.
MWANAMKE
mmoja wa Kitanzania aliyefanya ukabaha kwa miaka 18 katika miji
mbalimbali ya Tanzania, likiwemo Jiji Kuu la kibiashara la Dar es Salaam
na mingine ya Namibia, ameibuka na kueleza jinsi alivyotenda dhambi ya
kusambaza Ukimwi kwa wanaume wakware.
Licha
ya kukiri kufanya hivyo, akisema kwa siku alipanga hadi wanaume
watano,tena bila ya kutumia kinga akisema alidhamiria kuusambaza ugonjwa
huo hatari alioambukizwa akiwa katika shughuli za ukahaba.
Alijigundua
ameathirika mwaka 2006. Hata hivyo, katika maelezo yake ameelezea
kuijutia dhamira yake hiyo, akisema alisambaza kutokana na hasira
aliyokuwa nayo dhidi ya mwanamume aliyemwambukiza.
“Nilimchukia
sana kila mwanamume, yeyote aliyejiita mwanamume…nilishindwa tu
kuwawinda na kuwaua, lakini dhamira yangu ilikuwa kutumia silaha yoyote
kuua wanaume kwa sababu mmoja wao aliniua…
“Ndani
mwangu nilijisemea kamwe sitawaambia hali ya afya yangu, yeyote
anayekuja kwangu nammaliza. Kwa namna walivyoniambukiza lazima
niwaambukize’.
“Sijui nimewaambukiza wanaume wangapi, lakini ni maelfu,” alisema mwanamke huyo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 32, alipotoa ushuhuda wake kanisani nchini Nigeria hivi karibuni.
Comments
Post a Comment