Waziri Makalla haibu tupu…Dar-es-laam!
Naibu waziri wa maji Amos Makalla amehaibika mbeleya wafuasi wake baada ya
kuzuka vurugu kali kati ya wafuasi wa CCM na CHADEMA .
PICHANI: GARI YA WAZIRI MAKALLA IKIWA KATIKA ULINZI MKALI WA FFU. |
Katika fujo hizo zilizotokea hapa Kinondoni jijini Dar-es –laam
wana CCM na wapinzani wao CHADEMA walionekana kutoleana maneno machafu huku
kila mmoja akijaribu kujisafisha kwa mwenzake.
Kitendo kilitokea baada ya waziri huyo kusimama na kuanza kuzungumzia
ilani ya chama, ghafla wana CHADEMA walikasirika na kuanzisha fujo ambazo
kimsingi zilionekana azinamantiki kwa baadhi ya wanachama wa CCM ndipo minong’ono ilipoanzia na baadae
kupigana.
Baadae jeshi la polisi liliingilia kati japo halikuweza
kutegua kitendawili mpaka pale walipoamua kumuondoa waziri Makalla kutoka
katika kiwanja cha Goba jijini hapa.Baadae aliojiwa na waandishi wa habari ambapo alisema
yafuatayo.” haya niliyatarajia kwa hiyo siwezi kushangaa….. ”
polisi wakipambana na wana CHADEMA katika viwanja vya Goba, jijini Dar-es-laam. |
Kwa upende wake mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema
hayayamepangwa kupinga majukuma ya kutoa huduma ya maji jimboni hapa.Hii ndiyo Tanzania.
Comments
Post a Comment