Maajabu India:Kijana ang'olewa meno 232
Maajabu:Kijana ang'olewa meno 232
Madaktari nchini India wametumia
 saa 7  kufanikisha upasuaji wa kinywa cha kijana Ashik Gavai mwenye 
umri wa  miaka 17 aliyekuwa akipata maumivu ndani ya kinywani .
Dr Sunanda Dhiware, mkuu wa Kitengo cha tiba ya meno katika hospitali ya JJ mjini Mumbai ameiambia BBC kuwa wamefanikiwa kuyang’oa meno 232 kinywani mwa Ashik aliyeletwa hospitalini hapo akiwa amevimba taya huku akilalamika kwa maumivu makali.
Madaktari wamesema wamelazimika kutumia nyundo 
na tindo  kuyatoa meno hayo na wakadai kwamba  hilo ni tukio la ajabu na
 linaingia katika  rekodi ya dunia.Hata hivyo Upasuaji huo umehusisha 
jopo la madaktari wanne.
Dr Dhiware anasema katika uzoefu wake wa miaka 
30 ya udaktari wa kinywa na meno hajawahi kukutana na tukio la namna 
hiyo. Ameongeza pia kuwa kulingana na vitabu vilivyopo vinasema hali 
kama hiyo inaweza kujitokeza katika taya la juu na meno yaliyowahi 
kung'olewa katika hali hiyo yalikuwa 37 lakini cha kushangaza ni kuwa 
tukio la Ashik Gavai limetokea katika taya ya chini na ameng'olewa meno 
232 idadi ambayo ni kubwa huku akisalia na 28 kwa matumizi yake ya 
kawaida wakati kitaalamu mtu mzima anapaswa kuwa na meno 32.
Baba mzazi wa kijana Ashik ,Suresh Gavai 
amenukuliwa akisema mtoto wake alikuwa akilalamika kwa miezi kadhaa juu 
ya maumivu na kwamba  walidhani inaweza kuwa ni matatizo ya saratani na 
ndipo wakamleta Mumbai.
 
 
 
Comments
Post a Comment