Mbunge wa KIGOMA Kusini, ni ukweli mtupu huo!.
Login
WAKATI Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi),
David Kafulila, akifunguliwa kesi namba 131/2014 na Kampuni ya
kuzalisha Umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wenzake
wawili, kwa madai ya kutoa tuhuma za wizi wa tsh Bilioni 200 kutoka
kwenye akaounti ya Escrow iliyofunguliwa na Serikali kwa ajiri ya
kutunza fedha za kuilipa IPTL kwa kuzalisha umeme wa dharura.
Hata hivyo Mbunge huyo amesema hajapata taarifa rasmi za
kufunguliwa kesi ya madai ya Sh. bilioni 310 mahakamani, na kwamba
wanaruhusiwa kufanya hivyo kwakuwa wana haki kisheria pamoja na kwamba
wao ndiyo wezi wa pesa hizo.
Kafulila ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho Chama Chake
kimeanza ziara ya nchi nzima ikiwa na ujumbe wa 'Bring back our money'
rudisha pesa zetu ikiwa ni kuishawishi serikali kusimamia wizi huo ili
pesa hizo ziweze kurudishwa kwa wananchi badala ya kutafunwa na wajanja
wachache wakati zinatokana na kodi za wananchi.
Mbali na NCCR- Mageuzi kumfukuza Mbunge huyo na kumvua
uanachama kabla ya kurudishwa Bungeni kwa amri ya Mahakama, kama ilivyo
kwa Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,pamoja Hamad
Rashd wa CUF walivyo fukuzwa, lakini wakarudishwa Bungeni kwa nguvu ya
Mahakama.
katika suala hili Kafulila na Chama chake hicho cha zamani wameendelea kushirikiana na kuwa pamoja katika suala hilo.
Comments
Post a Comment