SHILOLE NA MZIWANDA NDANI YA SHELA HIVI KARIBUNI,...WANAFIKI KIMYA!.
SHILOLE |
Msanii
wa maigizo na muziki wa kizazi cha leo, Zena Mohammed
'Shilole' amekuja juu na kusema anashangazwa na habari
zilizozagaa mjini kuwa yeye amekataliwa ukweni....
Akiongea na Mpekuzi, Shilole amesema: "Nashangaa
watu wanasema eti nimekataliwa ukweni kisa umri wangu kuwa
mkubwa kuliko wa mwanaume. Ninachokijua mimi umri haujalishi
katika mapenzi, kikubwa ni upendo wa kweli na kuheshimiana.
"Habari
za mimi kukataliwa ukweni hazina ukweli wowote, na wala hakuna
mtu niliyezungumza naye kuhusiana na hilo swala na wala
hakuna ndugu yeyote wa Nuh Mziwanda aliyeonysha kutonipenda.
"Nilipokelewa
kwa furaha sana Ukweni na habari njema ni kwamba hivi
karibuni mtarajie kuona ndoa ili wanafiki tuwafunge midomo
yao," alisema Shilole.
Comments
Post a Comment