BBC KUPIGWA MARUFUKU NCHINI RWANDA, KURA YA MAONI YAENDELEA
 Bunge nchini Rwanda limepiga kura ya  kupiga marufuku BBC nchini humo, kufuatia kipindi maalum cha  Televisheni kilichoitwa ''Untold story'' kuhusu mauaji ya kimbari ya  mwaka 1994 kilichopeperushwa na BBC.  Kipindi hicho kilihoji uhusika wa baadhi ya maafisa wakuu serikalini juu ya yale yaliyotokea wakati wa mauaji ya kimbari.  Bunge  hilo linataka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya BBC kwa kupeperusha  kipindi hicho ambacho wanasema kinahujumu mauaji ya Kimbari na pia  kukana mauaji dhidi ya watutsi.