BIG UP ARTEL KWA KUWAKUTANISHA WASANII WA BONGO NA WASANII WA NJE.
Mwanamuziki
wa kizazi kipya, Ommy Dimpoz (kushoto) akizungumza na Ofisa Uhusiano wa
Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (katikati) huku mdada flani kutoka
Airtel akiwasikiliza.
Mshereheshaji
katika hafla hiyo, Ephrahim Kibonde, (kushoto) akionesha headphones
baada ya kutangaza shindano la kuimba kwa waliohudhuria hafla hiyo ya
uzinduzi. Kulia ni wadada warembo waliokuwa wakiwahudumia wageni
waalikwa.
KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Airtel, juzi, Ijumaa ilizindua shindano
liitwalo Airtel TRACE ambapo mtumiaji wa mtandao wa Airtel atatakiwa
kupiga namba 0901002233 na kuimba nyimbo zake kupitia kwenye simu yake ambazo zitasikilizwa na majaji.Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika ukumbi wa High Spirit, uliopo Jengo la IT Plaza, Posta jijini Dar, Meneja Masoko wa Airtel Tanzania, Aneth Muga, alisema mshindi atakayepatikana hapa nchini atakwenda kushindanishwa na washindi wengine kutoka nchini 13 za Afrika ili kumpata mwimbaji bora wa Afrika.
Mshindi atakayepatikana barani Afrika atakwenda kuungana na msanii nyota wa Marekani Akon na kupiga nae kazi.
Comments
Post a Comment