Rais wa Zanzibar,Amteua Mwanasheria Mkuu Zanzibar
hongera!
 Mhe Said Hassan Said Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
                            
                                                        
                                                        
                            Mhe Said Hassan Said Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Tuesday, October 7, 2014
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
 Shein, amefanya Uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi 
Zanzibar, kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya  Kifungu 55(1)cha Katiba
 ya Zanzibar ya 1984, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amemteuwa Mhe, 
Said Hassan Said kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Uteuzi huo umeaza 
leo 7,Oktoba 2014. Kabla ya uteuzi huo Mhe, Said Hassan Said alikuwa 
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mhe, Said Hassan Said, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu
 wa Zanzibar Mhe, Othman Masoud Othman ambaye uteuzi wake umefutwa kwa 
mujibu wa Vifungu vya 53,54 (1) na 55(3) vya Katiba ya Zanzibar ya 1984 
na kifungu 12 (3) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Namba 2 ya 2011.  
 
 
 
Comments
Post a Comment