MAJONZI MAZITO YAMFIKA ALII.
Ali Choki akipozi
MKURUGENZI wa bendi ya Extra Bongo, Ali Choki
amepata pigo la kuondokewa na mke wake, Shuea Hamis ‘Mama Shuu’ baada ya
kuugua kwa muda mrefu Usiku wa kuamkia leo.Akizungumza kwa masikitiko Ali Choki alisema mke wake ameugua kwa muda wa miezi tisa akiwa anasumbuliwa na mguu ambapo alitibiwa nchini India ikashindikana akarudishwa nyumbani mpaka mauti yalipomfika usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
“Ukweli nimeumia kwani mke wangu ndiye aliyekuwa mshauri wangu mkuu na ndiye kila kitu kwangu alikuwa akinisapoti kwenye kazi yangu ya muziki lakini ndiyo hivyo Mungu amempenda zaidi sina la kufanya,”alisema Ali Choki.
Aidha Choki alisema mipango ya mazishi ilifanyika nyumbani kwao Tuangoma Kigamboni na mazishi ya mkewe yalifanyika jana Jumapili saa kumi jioni katika makaburi ya Chang’ombe Madukamawili.
(Habari na Gladness Mallya)
Mambobomba inawapapole ndugu jamaa na marafiki pole sana Alii.
Comments
Post a Comment