UN:Ebola kudhibitiwa kwa miezi mitatu
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ugonjwa wa Ebola David
Nabarro ameiambia BBC kuwa mlipuko wa ugonjwa huo magharibi mwa Afrika
unaweza kudhibitiwa katika kipindi cha miezi mitatu.
Dr.Nabarro alisema kuwa ina maana kuwa visa vipya vya ugonjwa huo vitapungua kila wiki.Nabarro amesema kuwa kuuelewa ugonjwa wa Ebola miongoni mwa jamii zilizoathirika kutasaidia kupambana nao kwa kuwa watu wanaelewa kwamba kuwatenga wagonjwa ndiyo njia bora ya kuzuia maambukizi.
Zaidi ya watu 4000 wameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola wengi kutoka mataifa ya Sierra Leone, Liberia na Guinea.
Comments
Post a Comment