KWA NINI WANAWAKE WANA WIVU AMBAO HAUNA TIJA?.
Uzuri wamponza dada huyu
WASICHANA ndugu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 16 na 18 wamemshambulia kwa visu binti mwenye miaka 15, kwa lengo la kumkomesha kwa sababu anasifiwa kuwa mzuri.
Katika
 tukio hilo la aina yake, ndugu hao walimvizia msichana huyo, Julia 
Alvarez(15), njiani wakati anakwenda nyumbani mjini Juan Domingo Peron 
kwenye jimbo la Formosa Kaskazini mwa Argentina.
Kwa
 mujibu wa kauli za wasichana hao, walifanya unyama huo kwa kuwa 
hawakupenda kusikia sifa alizokuwa anapewa binti huyo kuwa ni mrembo 
sana.
Mwathirika
 huyo, Alvarez alisema wakati anashambuliwa, wasichana hao walisema, 
walitaka kumharibu awe anatisha kama mcheza sinema za kutisha, Chucky.
Msichana
 huyo alisema alivamiwa wakati anakwenda nyumbani kujiandaa kwenda 
kuwatembelea rafiki zake, wasichana wawili walimvamia, wakaanza kumpiga 
na kumwangusha chini. Alvarez amesema, baada ya yeye kuanguka, wasichana
 hao walitoa visu na wakasema,
“Kila
 mtu anasema una mvuto, tukikumaliza mvuto wote utaisha, watu watakuita 
Chucky”. Mtoto huyo alikatwa kwa visu kwenye sehemu mbalimbali mwilini 
hasa usoni na mgongoni. Baada ya kumuumiza binti huyo, wasichana hao 
walikimbia na kumwacha amelala kwenye dimbwi la damu, mpita njia 
alimwona, akamkimbiza hospitali.
Inadaiwa
 kuwa, awali polisi hawakuchunguza tukio hilo lakini dada wa majeruhi 
aliweka picha za mdogo wake kwenye mtandao wa facebook, ndipo watu 
wakashinikiza haki itendeke. Wasichana waliomshambulia Alvarez 
wakamatwe.
“Walimwonea
 wivu mdogo wangu kwa muda mrefu, na kila mara walimkashifu na kumtukana
 lakini hatukutarajia kufika mbali kiasi hiki. Nimejaribu kuwa mvumilivu
 kwa ajili ya mdogo wangu mrembo lakini kila mara nikimwona nataka 
kutokwa machozi, wameharibu maisha yake,” amesema mwanamke kwenye ukurasa wa facebook akijitambulisha kuwa ni dada wa binti aliyejeruhiwa.
“Alisema anataka kujiua kwa sababu sasa akijitazama kwenye kioo anajiona mbaya, imeharibu familia yetu,” alieleza mwanamke huyo.
 Mambobomba inawaasa wanawake wawe wavumilivu wenye kutafakari kabla ya kutenda.

 
 
 
Comments
Post a Comment