MASHINDANO YA UMISS YARUHUSIWA MAHAKAMANI NCHINI TANZANIA
MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es Salaam, jana iliamuru mashindano
ya urembo Tanzania yaliyopangwa kufanyika Oktoba 11, mwaka huu kuendelea
baada ya kutupilia mbali maombi ya dharura yaliyowasilishwa na Prashant
Patel dhidi ya Hashimu Lundenga ya kuzuia kuendelea kuendesha
kinyang’anyiro hicho kwa madai ya kukiuka mkataba wa makubaliano yao.
Kadhalika
mahakama hiyo imesema maombi ya hati ya dharura yaliyowasilishwa na
Patel hayana mashiko ya kisheria na kwamba kuzuia kufanyika mashindano
hayo ambayo wadhamini mbalimbali wamewekeza fedha zao itasababisha
mgongano wa kimaslahi.
Uamuzi
huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Frank Moshi baada ya kusikiliza
hoja za mawakili wa pande zote mbili kuhusu maombi hayo ya dharura ya
kuzuia mashindano hayo kufanyika Oktoba 11, mwaka huu.
Hakimu
Moshi alisema mlalamikaji amefungua kesi mahakamani hapo pamoja na
maombi ya hati ya dharura akiitaka mahakama yake kuzuia mashindano
kufanyika kutokana na mlalamikiwa kuvunja haki dhidi ya mwanzilishi
mwenzake Patel.
Alisema
Patel kupitia hoja za maombi yake, amedai kuwa Lundenga alivunja
mkataba huo kwa kufanya mawasiliano moja kwa moja na mawakala bila
kumshirikisha.
Hata
hivyo, mahakama bila kuacha shaka imeona hakuna sababu za msingi katika
hati hiyo ya kusababisha mashindano hayo yasifanyike na kwamba hayawezi
kuathiri kesi ya msingi iliyofunguliwa na mlalamikaji huyo.
“Mahakama
imeona hakuna sababu ya kuzuia mashindano hayo kwa sababu wadhamini na
washiriki wametumia gharama zao na kwamba kwa kufanya hivyo
kutasababisha mgongano wa kimaslahi” alisema Hakimu Moshi wakati
akitupilia mbali hati hiyo ya dharula.
Akifafanua
zaidi alisema hati ya dharura ya mlalamikaji haina mashiko kisheria kwa
sababu kesi yake ya msingi ipo mahakamani na kwamba haina uhusiano na
mashindano yatakayofanyika Oktoba 11, mwaka huu.
Mapema juzi, mahakama hiyo ilitupilia mbali pingamizi la awali la Lundenga lili
Comments
Post a Comment