BBC KUPIGWA MARUFUKU NCHINI RWANDA, KURA YA MAONI YAENDELEA
Bunge nchini Rwanda limepiga kura ya
kupiga marufuku BBC nchini humo, kufuatia kipindi maalum cha
Televisheni kilichoitwa ''Untold story'' kuhusu mauaji ya kimbari ya
mwaka 1994 kilichopeperushwa na BBC.
Kipindi hicho kilihoji uhusika wa baadhi ya maafisa wakuu serikalini juu ya yale yaliyotokea wakati wa mauaji ya kimbari.Bunge hilo linataka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya BBC kwa kupeperusha kipindi hicho ambacho wanasema kinahujumu mauaji ya Kimbari na pia kukana mauaji dhidi ya watutsi.
Comments
Post a Comment