EBOLA YAISHAMBULIA MAREKANI TENA MUUGUZI MMOJA AGUNDULIKA NA VIRUSI.

EBOLA INAENDELEA KUWA GUMZO HATA PAMOJA NA BAADHI YA KAULI CHAFU ZA MSANII CHRIS BROWN KUSEMA HII NI NJIA NZURI YA KUPUNGUZA ONGEZEKO LA WATU NAJUA ALISEMA KWA SABABU ALIKUWA NA KIBURI KUWA YUKO KATIKA TAIFA TAJIRI ILA JANGA NI JANGA LAWEZA KUMFIKA TAJIRI HAMA MASKINI AMA MTU YEYOTE.

Muguzi mwingine wa afya mwenye umri wa miaka 26 nchini Marekani amepatikana na ugonjwa wa Ebola katika jimbo la Texas.

Maafisa wa afya wanasema muuguzi huyo tayari anapokea matibabu baada ya kuambukizwa ugonjwa huo na mwanamume raia wa Liberia aliyefariki kutokana na ugonjwa huo wiki jana.

Maafisa nchini Marekani wanasema wanawachunguza watu wengine 48 waliokaribiana na raia mgonjwa aliyefariki na Ebola wakiwemo wahudumu wa afya waliomtibu.

Shirika la afya duniani linasema watu 4,447 wamefariki na Ebola, hasa katika mataifa ya Afrika Magharibi.

Nina Pham alimtibu raia wa Liberia aliyekuwa mtu wa kwanza kuugua Ebola nchini Marekani Thomas Duncan. Alifariki akipokea matibabu.

Madaktari walisema kuwa muuguzi huyo yuko katika hali nzuri tangu Jumanne.

Muuguzi wa pili kuambukizwa Ebola hajatajwa , hata hivyo inaarifiwa pia alimhudumia bwana Duncan alipokuwa hospitalini.

Aliwekwa karantini mara moja baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa wa Ebola.

Comments

Popular posts from this blog

STYLE KALI:TUMIA HII NDANI YA DAKIKA MOJA TU MWANAMKE AMEKOJOA.

KISIMI (kinembe) kikichezewa mwanamke anaweza kuwataja maawara zake wote.