EBOLA JANGA LA HATARI, UN.KASI YA MAAMBUKIZI YAWA MOTO SANA.
Afisaa mkuu wa Umoja wa Mataifa
kuhusiana na janga la Ebola, anasema kuwa dunia inajikokota katika vita
vyake dhidi ya Ebola huku maelfu ya watu wakiwa katika hatari ya
kuambiukizwa ugonjwa huo ifikapo Disemba mwakani.
Afisaa huyo
Anthony Banbury ameambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwamba
kasi ya maambukizi ya Ebola ni ya kutisha na kwamba, huenda
ikashindikana kudhibiti maambukizi.Wakati huohuo, idadi ya watu waliofariki kutokana na Ebola tangu janga hilo kuanza imefika 4,447 , wengi wakiwa katika kanda ya Afrika Magharibi.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani, WHO.
Naibu mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bruce Aylward, pia alisema huenda watu 10,000 wakaambukizwa ugonjwa huo kila wiki kwa kipindi cha miezi miwili ikiwa juhuudi za kimataifa haziongezwa kasi kupambana na ugonjwa huo.
Lakini kiwango cha maambukizi mapya katika baadhi ya maeneo kimepungua.
Sierra Leone, Liberia na Guinea, ndizo nhi zilizoathirika zaidi kutokana na ugonjwa huo tangu kuanza kwake.
Katika matukio mengine:
Uingereza imeanza kuwakagua na kuwachunguza watu katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Heathrow
Daktari wa kikosio cha wanajeshi wa kulinda amani wa Siera Leone alipatikana na Ebola mjini Freetown.
Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kutoka Sudan alifariki nchini Ujerumani baada ya kuambukizwa Ebola nchini Liberia.
Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg amesema yeye na mkewe Priscilla Chan, watachanga dola milioni 25 za kusiadia vita dhidi ya Ebola.
Muuguzi mmoja wa Uhispania, alikuwa mtu wa kwanza kuugua ugonjwa huo nchini Hispania na angali yuko hali mahututi, ingawa madaktari wanasema ana dalili za hali yake kuimarika.
Comments
Post a Comment