EBOLA;KINGA YA EBOLA YAANZA MAJARIBIO HUENDA IKAWA SULUISHI.
Shirika
la afya duniani leo linaongoza mkutano wa kamati yake ya dharura ,
kutathmini hali ya hivi karibuni kuhusiana na mlipuko wa Ebola .
Mkutano
huo unafanyaika wakati ugonjwa huo ukiendelea kuenea katika nchi tatu
zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa huo Guinea, Sierra Leone na Liberia -
ingawa Senegal na Nigeria, ambazo zilikuwa na visa vichache zimetangazwa
kutokuwa na ugonjwa huo.
Ni mara ya tatu sasa kamati ya dharura ya WHO inakutana .Lengo la sasa ni kutathmini juhudi zilizofikiwa za kudhibiti ugonjwa huo na kuuzuia kuenea.
Kamati hiyo itaangalia hatua zilizopo za uchunguzi wa
mlipuko huo katika mipaka. Je hatua hizo zinafaa, na je yaweke masharti
kamili ya kusafiri kwenye maeneo hayo ?
Kuna baadhi ya sababu
ndogo za kuwa na matumaini - kwa pamoja Nigeria na Senegal zimeweza
kuzuia kuenea kwa visa vya Ebola . Na awamu ya kwanza ya kinga za
majaribio zinazoweza kuaminika zinatarajiwa kuwasili Geneva hii leo .
Lakini kinga kamili zilizoidhinishwa dhidi ya Ebola huenda zikapatikana miezi kadhaa ama baada ya mwaka
Comments
Post a Comment