BAADA YA RISIMU YA KATIBA MPYA KUWIVA UKAWA WAIBUA MAPYA.
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeibua shutuma dhidi ya uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba kwamba unawarubuni kwa fedha baadhi ya wajumbe wa umoja huo ili kuipigia kura Katiba inayopendekezwa.
Kamati ya Ufundi ya Ukawa, ilisema jana kuwa wajumbe wanaorubuniwa 
wapige kura ya ‘ndiyo’ kwa ahadi ya kupewa zaidi ya Sh500 milioni ni wa 
CUF na wengine wanne wa Chadema wanaotoka Zanzibar.
Hata hivyo, Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Khamis Hamad alikanusha 
madai hayo, akisema hajasikia kitu kama hicho na ndiyo kwanza alikuwa 
anasikia hilo kutoka kwa mwandishi wa habari hizi… “Hakuna kitu kama 
hicho, hilo jambo ndiyo nalisikia kutoka kwako.”
Kutokana na madai hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ukawa, John Mnyika 
alisema kamati hiyo ilianza kikao cha siku mbili kuanzia jana kujadili 
hali hiyo na kutoa mapendekezo kwa uongozi wa juu wa umoja huo.
Licha ya Mnyika kukataa kutaja majina ya wajumbe waliorubuniwa, 
wajumbe wa Chadema wanaotokea Zanzibar ni Zeudi Abdallah ambaye pia ni 
Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Maryam Msabaha, 
Mwanamrisho Abama na Raya Ibrahim. “Tumewataka wajumbe wetu wote 
kukusanya ushahidi na kuuwasilisha kwa viongozi wa Ukawa,” alisema 
Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema 
Bara.


Aliongeza, “Chadema ina wajumbe wanne, watatu ni wabunge wa kawaida 
na mmoja wa kuteuliwa na Rais (Kundi la 201). Tumepata taarifa kutoka 
kwa wajumbe hao kwamba wanapigiwa simu na uongozi wa Bunge ukiwataka 
wasaini karatasi za kupigia kura ili uongozi wa Bunge uchakachue kura.
“Tumeanza kikao kujadili suala hili ila tumeamua kwanza tuueleze umma kupitia vyombo vya habari juu ya ‘uharamia’ unaofanywa na Bunge la Katiba linaloongozwa na Sitta (Samuel) na Makamu wake Samia (Suluhu Hassan).”
Ukiukaji kanuni
Akinukuu Kifungu cha 36 (3) cha Kanuni za Bunge la Katiba, Mnyika 
alisema si sahihi Sitta kutaka wajumbe waliopiga kura ya ‘hapana’ kuitwa
 katika Kamati ya Mashauriano na uamuzi huo ni kinyume na kanuni…
“Ni kama kuwatisha tu wajumbe.”
Kanuni hiyo inasema; “Endapo baada ya ibara ya Rasimu ya Katiba 
iliyopendekezwa upya kupigiwa kura, theluthi mbili ya wajumbe wote 
kutoka Tanzania Bara na theluthi mbili ya wajumbe wote kutoka Tanzania 
Zanzibar haikufikiwa, basi ibara hiyo itapelekwa kwenye Kamati ya 
Mashauriano ili kupata mwafaka.”
Sitta awataje
Mjumbe mwingine wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha wa 
CUF, Joran Bashange alimtaka Sitta kutaja majina ya wajumbe wa CUF na 
Chadema waliopiga kura… “Tunamtaka awataje kwa majina maana ujanja wake na wenzake tumeshaujua na tuna ushahidi wote.”
Bashange alisema mpaka sasa hakuna mjumbe wa Bunge hilo ambaye ni 
mjumbe wa Ukawa aliyepiga kura kupitisha Katiba inayopendekezwa.
“Ndiyo maana walibadili kanuni ili kuruhusu wajumbe kupiga kura kwa faksi na baruapepe ili kufanya ‘uharamia’ wa kuiba kura,” alisema.
Tupe maoni yako hapo Chini..!!
 
 
 
Comments
Post a Comment