DANGURO LA GUNGULIKA SHULENI
Stori: Richard Bukos na Issa Mnally
Ile Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ikishirikiana na askari wa ulinzi shirikishi, wamefanikiwa kufumua danguro hatari linaloendesha shughuli zake katika eneo la shule baada ya kumnasa mwanamke aliyedai ni mke wa mtu akifanya uzinzi na njemba ambaye hakujulikana jina lake.
Tukio hilo la aibu ya karne lilijiri ndani ya eneo la shule ya msingi
Shekilango, iliyopo Mapambano, Sinza jijini Dar, hivi karibuni ambapo
mke huyo wa mtu alikuwa akichepuka.Ile Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ikishirikiana na askari wa ulinzi shirikishi, wamefanikiwa kufumua danguro hatari linaloendesha shughuli zake katika eneo la shule baada ya kumnasa mwanamke aliyedai ni mke wa mtu akifanya uzinzi na njemba ambaye hakujulikana jina lake.
Awali, OFM ilipokea taarifa za kuwepo kwa uchafu huo kutoka kwa wasamaria wema wanaoishi eneo hilo baada ya kukerwa na tabia hiyo chafu huku wakiacha kondom zikiwa zimezagaa na kuhatarisha afya za watoto wao ambao huchezea mipira hiyo ya kinga kama mapulizo.
Baada ya OFM kunyetishiwa ishu hiyo, walishirikiana na askari hao ambapo walivamia eneo hilo na kumbamba mwanamke huyo akibanjuka na njemba.
Wawili hao, baada ya kubambwa 'laivu' walitiwa kizuizini kabla ya vijana wanaodaiwa kuchukua posho kwa wanaofanyia mambo yao kwenye danguro hilo kuanzisha vurumai ingawa walidhibitiwa huku jamaa aliyekuwa anahudumiwa akitoka nduki.
Akizungumza na gazeti hili, mwanamke huyo aliomba asamehewe na kusema kwamba kinachomsababishia kufanya shughuli hiyo ni ugumu wa maisha na kundi la watoto anaowalea ambao baba yao hana ajira.
Gazeti hili lilipotaka kuzungumza na mumewe ili kujua kama anafahamu kuwa mkewe anafanya biashara haramu ya kuuza mwili, mwanamke huyo alidai kwamba mumewe hana simu.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisikika akisema: "Dah! Mngewahi dakika kumi tu, mngemkuta baba wa Kiarabu aliyeingia na mwanamke muda si mrefu, hili danguro linatumiwa usiku kucha, yaani linapoingia giza tu hapa ni balaa hadi asubuhi."
Mwalimu wa zamu, Kilavo Charles, aliiambia OFM kuwa suala hilo limeshafikishwa kituo cha Polisi Mabatini ambao waliahidi kulishughulikia.“Ni aibu, asubuhi watoto wanafagia kondom, tunakosa cha kuwaambia, hii ni hatari kwa kweli na tunaomba mamlaka zinazohusika zilifanyie kazi jambo hili,” lisema.
JIUNGE NA SIMU DOKTA SASA UPATE USHAURI KUHUSU AFYA YAKO
Comments
Post a Comment