WAZIRI MKUU MH.MAZENGO PINDA AMEHITIMISHA ZIARA YAKE LEO.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na baadhi ya viongozi wa chama cha Walimu
Tanzania kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuhutubia katika
sherehe za siku ya walimu duniani zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa
Kaitaba mjini Bukoba Oktoba 5, 2014.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mbunge wa Bukoba Mjini, Hamisi
Kagasheki kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kabla ya kuondoka kuelekea
Dodoma Oktoba 5, 2014. Mheshimiwa Pinda alikwenda Bukoba kumwakilisha
Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za siku ya Walimu Duniani
zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Kaitaba.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma ya Kihaya kabla ya kuondoka kwenye
uwanja wa ndege wa Bukoba Oktoba 5, 2014 ambako alikuwa mgeni rasmi
kwenye sherehe za siku ya walimu duniani zilizofanyika kitaifa kwenye
uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Oktoba 5, 2014. Wengine kutoka kushoto ni
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa na Mbunge wa Luangwa, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa
Kagera, Kanali Mstaafu, Fabiana Massawe.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali
Mstaafu , Fabian Massawe (kushoto kwake) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa
Kagera, Costansia Buhiya (kulia kwake) kuvuka uwanja wa ndege wa Bukoba
baada ya kutua kwenye uwanja huo, Oktoba 4, 2014 ambako Oktoba 5,2014
alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya walimu duniani
zilizofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Comments
Post a Comment