CHAMA CHA MAPINDUZI NDANI YA DODOMA MAPAMBANO YA KIUCHUMI
Mwenyekiti wa
CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipanga makabrasha tayari
kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambapo masuala ya kujiendesha
kiuchumi na mipango ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa
yanajadiliwa.
Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa
NEC mjini Dodoma ambapo aliwaeleza juu ya kikao cha Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Oktoba 16, 2014 katika siku ya
kwanza ya kikao chake cha siku mbili kinachoendelea mjini Dodoma chini
ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili na kupitisha
Sera ya CCM ya kujitegemea kimapato na kiuchumi.
Comments
Post a Comment