Majanga mazito,Mtoto wa Miaka 9 afariki Dunia baada ya kujinyonga.
Katika hali ya kushangaza, mtoto Focus Saimoni (9), mkazi wa Kwa Bibi Yuda, Kinondoni jijini Dar amekutwa amejinyonga kwenye komeo la mlango wa sebule yao.
Focus
 aliyekuwa akisoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, 
amedaiwa kufanya tukio hilo Jumamosi iliyopita kwa kufunga gauni la 
mdogo wake shingoni na kujitundika kwenye komeo hilo mpaka kukata roho.
Kwa
 mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea saa 6 mchana wakati 
wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na kuacha ufunguo kwa mmiliki wa 
nyumba aliyejulikana kwa jina la mama Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa 
siku ya tukio,  Focus alirejea nyumbani kutoka shuleni na kumuacha mdogo
 wake, Irene Steve (5).
“Alipofika alichukua ufunguo kwa mama mwenye nyumba na kuingia ndani, akanywa chai. Baada ya muda, mdogo wake (Irene) alirudi na kumkuta tayari ananing’inia kwenye komeo la mlango,” kilisema chanzo.
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia.
“Nilimwambia
 Focus usinitanie mbona hauzungumzi na mimi, nilipomwangalia vizuri 
ndipo nikaona ana damu mdomoni, nikakimbia kwa mama mdogo anayeishi 
jirani na kumueleza,’’ alisema Irene.
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria alisema naye hakuamini tukio hilo.
  
“Aliponiambia Focus kaning’inia mlangoni nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.
  
“Ila mimi naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine.

Akizidi
 kufafanua juu ya mazingira aliyoyakuta, Catherine alisema alishangaa 
wakati akihangaika kuita majirani, aliporudi  aliukuta mwili umeshushwa 
chini.
 
“Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna aliyenijibu,’’ alisema Catherine.
  
Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo.

’’Tukio
 hili lina shaka ndani yake, mtoto wa miaka 9 anawezaje kujinyonga, kwa 
stress zipi? Kwa kweli inasikitisha sana, jeshi la polisi lina wajibu wa
 kuchunguza ukweli wa kifo cha mtoto huyo,” alisema mama huyo.
  
Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo pia walionekana kushtushwa na tukio hilo na kuwauliza wazazi kama mtoto huyo alikuwa na stress zozote?
Baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo pia walionekana kushtushwa na tukio hilo na kuwauliza wazazi kama mtoto huyo alikuwa na stress zozote?
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.
Mambobomba inatoa pole kwa wazazi wa marehemu Focus Saimon. 

Comments
Post a Comment