JE, BIFU LA DIAMOND NA ALI KIBA WIVU WA KIMAENDELEO AU NI VITA BARIDI? PATA KAULI ZAO HAPA.
MHARIRI,

“Unajua kuna time ikifika inabidi uangalie na kuna vitu uvizoee tu sababu havikuanza leo hivi vitu sio tu kwa Ali, ukiwa unafanya vizuri ni msanii yeyote ambaye atakuwepo nae anafanya nyimbo au akatoa nyimbo yaani utakuja utashindanishwa nae tu, atakuja huyu na huyu na huyu, lakini wewe mwenyewe tu kuangalia heshima yako iko wapi kuangalia kazi zako unazifanyaje ubora wake”.
  
“Hata kwenye boxing ipo, ukiangalia hata kuna kipindi ilikuwa TMK na East Coast, ilikuwaga kwa Dully na T.I.D hivi ni vitu vya kikazi hata kwenye mpira ndio maana kuna Simba na Yanga, lakini haimaanishi Simba na Yanga ni maadui wakikutana Ngassa ntakupiga ngumi au flani ah ah..”
  
“Ukiniuliza mimi kiundani kabisa siamini kama kutakua na tatizo la damu ya mtu na mtu, bali ni vitu ambavyo vipo vya kisanaa au vya kimashabiki kwa mashabiki. Mi nasisitiza sana media na watu wasitengeneze kufanya kama ni matatizo ya mtu na mtu kwasababu kisanaa inakua haijengi, lakini inapokuwa ni baina ya kazi na kazi inakua inasaidia kwasababu inafanya watu wawe na changamoto ya kusema ngoja nitoe kazi kali ili nifanye kitu kizuri inasababisha muziki wetu ukue.”
Diamond
 na Alikiba ndio wasanii wa bongo fleva wenye timu mbili kubwa za 
mashabiki waliogawanyika na kuwashindanisha kwa niaba yao, Team Diamond 
v/s Team Alikiba, ushindani ambao umevalishwa ‘mask’ za ‘beef’ ambayo 
Nasib Abdul amedai kuwa haipo.
Platnumz
 ambaye alikuwa bado hajaamua kuzungumzia tofauti hizo ameamua kufunguka
 juu ya ushindani pamoja na ‘beef’ iliyokuwa inazungumzwa baina yake na 
muimbaji huyo wa ‘Mwana’.
  
“Nimekua
 nikiskia muda mrefu vimezungumziwa sana, kwenye mitandao katika nini, 
sijui kwanini vinazungumziwa hivyo” aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm 

“Unajua kuna time ikifika inabidi uangalie na kuna vitu uvizoee tu sababu havikuanza leo hivi vitu sio tu kwa Ali, ukiwa unafanya vizuri ni msanii yeyote ambaye atakuwepo nae anafanya nyimbo au akatoa nyimbo yaani utakuja utashindanishwa nae tu, atakuja huyu na huyu na huyu, lakini wewe mwenyewe tu kuangalia heshima yako iko wapi kuangalia kazi zako unazifanyaje ubora wake”.
“Tangia
 mwanzo yaani inavyoanza ishagatokeaga hivyo ilikua sijui kwa Belle 9, 
ilitoka kwa Belle 9 ikaja nafikiri sijui Sam Wa Ukweli ilikua, ikaja 
sijui kwa Bob Junior, ikaja pia kwa Ali, ikatoka kwa Ali tena ikaja 
ikaondoka ikaenda kwa Omary I mean Ommy Dimpoz, ikatoka tena ikaja kwa 
Richard Mavoko, so kila time inavyokuwa inaenda unafanya vizuri hivyo 
vitu vinakua vinatokea, so ni we mwenyewe kuangalia na watu wasiokuwa na
 upeo wanaweza wakahisi hawa watu wana tatizo kumbe si tatizo ni vitu 
ambavyo vitakuwepo tu kwasababu mashabiki wana tabia wakiona mtu 
anafanya hichi na we unafanya kitu mkiwa katika kazi inayofanana hivyo 
vitu vitatokea yaani watu watashindanisha, unaweza hata ukashindanishwa 
na mtu ambae hata hakufikii kiwango kabisa”.
“Hata kwenye boxing ipo, ukiangalia hata kuna kipindi ilikuwa TMK na East Coast, ilikuwaga kwa Dully na T.I.D hivi ni vitu vya kikazi hata kwenye mpira ndio maana kuna Simba na Yanga, lakini haimaanishi Simba na Yanga ni maadui wakikutana Ngassa ntakupiga ngumi au flani ah ah..”
Diamond
 amesema kuwa kama Alikiba alikuwa na tatizo na yeye anaamini angeweza 
kumfata na kumwambia sababu amefahamiana nae kabla hajakuwa mwanamuziki.
  
“Sasa
 hivi yaani karibia mwaka wa tano, Mi tangia nianze kufanya muziki 
sijawahi kudrop kila siku nazidi kupanda juu…so hivyo vitu lazima 
vitatokea lazima nivikubali, inawezekana we unasema we unasema we hauna 
tatizo lakini mwenzio akawa anahisi wewe una tatizo nae, lakini naamini 
kama angekuwa anahisi kama mimi nina matatizo na yeye angenifata 
akaniambia kwa sababu mimi sijajuana na Ali kwenye muziki, nimejuana na 
Ali kabla sijakuwa mwanamuziki, nimemjua Ali kupitia dada yangu Queen 
Darleen so alikuwa an uwezo wa kunifata akaniambia personally kwamba 
bana umefanya hichi na hichi na hichi”.
  
Diamond
 amemaliza kwa kusema kuwaomba media na mashabiki wasifanye ionekane 
kama wana beef binafsi bali wazishindanishe kazi ili kukuza muziki wa 
Tanzania.
“Ukiniuliza mimi kiundani kabisa siamini kama kutakua na tatizo la damu ya mtu na mtu, bali ni vitu ambavyo vipo vya kisanaa au vya kimashabiki kwa mashabiki. Mi nasisitiza sana media na watu wasitengeneze kufanya kama ni matatizo ya mtu na mtu kwasababu kisanaa inakua haijengi, lakini inapokuwa ni baina ya kazi na kazi inakua inasaidia kwasababu inafanya watu wawe na changamoto ya kusema ngoja nitoe kazi kali ili nifanye kitu kizuri inasababisha muziki wetu ukue.”
maoni ya wahariri bifu la kimaendeleo
 
Comments
Post a Comment