EBOLA, KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA ATOA TAHARIFA KALI KWA MATAIFA YA MAGHARIBI.
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan mwenye nishani ya nobel amekosoa ambavyo mataifa ya mgahribi yameshughulikia janga la Ebola.
Bwana Annan ameambia BBC kwamba hajaridhishwa kamwe na hatua za mataifa ya magharibi kupambana na Ebola.
''Ikiwa janga hilo lingekuwa limeathiri eneo lengine , hatua ambazo zingechukuliwa zingekuwa toifauti sana.''
''Hata ukiangalia ambavyo janga hili limekuwa likienenea , mataifa ya magharibi yalichukua hatua tu wakati ambapo ugonjwa huo ulitambuiliwa katika mataifa yao kama vile Marekani na Ulaya.''
Kwiengineko, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezindua kampeini ya kuchagisha mamilioni ya dola kusaidia kwa vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola, baada ya kampeini ya awali ya kuchangisha pesa kukosa kufikia malengo yake.
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kampeini aliyozindua mwezi Septemba kuchangisha pesa imefanikisha tu mchango wa dola 100,000 kufikia sasa.
Ban Ki Moon ni mmoja wa viongozi wa kimataifa wanaokosoa juhudi za kimataifa za kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola akisema ni hafifu mno.
Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 4,500 kufikia sasa wengi wakiwa katika mataifa ya Liberia, Guinea na Sierra Leone.
Wadhamini wametoa mchango wa karibu dola milioni 400 kwa mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa lakini sio kwa kampeini aliyozindua bwana Ban ambayo inapaswa kuwa kama akiba ya pesa zitakazotumiwa kwa vita dhidi ya Ebola pindi zinapohitajika.
Kuna ahadi ya dola milioni 20 katika mchango zitakazotolewa kwa kampeini hiyo.
Kati ya mataifa ambayo yameahidi kutoa mchango wao kwa Ban Ki Moon ni Colom,bia pkeke ambayo tayari imetoa dola laki moja.
Mjumbe maalum wa Umoja huo kuhusu Ebola, David Nabarro, amesema hazina hiyo itakuwa afueni kwa vita dhidi ya Ebola ambavyo kwa sasa limegeuka na kuwa janga la kimataifa.
Bwana Ban amesema ni wakati kwa dunia nzima kuchukua hatua haya mataifa yenye uwezo mkubwa kutoa msaada wa kifedha na uwezo wa kuwafikia wagonjwa na pia kutoa matibabu.
Wito kama huo umetolewa katika siku za hivi karibuni na Rais wa Marekani Barack Obama , waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim.
Comments
Post a Comment