EBOLA;TECHNOLOGIA MPYA YA WHATS APP ITUMIKE KUDHIBITI EBOLA AFRIKA.
Watu wengi barani Afrika wanatumia huduma ya Whats App kutumiana ujumbe mfupi
BBC
imezindua huduma mpya ya umma ya kiteknolojia inayotoa taarifa za afya
kuhusiana na ugonjwa wa Ebola kupitia kwa programu ya kijamii ya kutuma
ujumbe mfupi kwenye internet ya 'WhatsApp.'
Programu hio inawalenga zaidi watumiaji wa Internet katika kanda ya Afrika Magharibi.Huduma hio itawezesha wasomaji kupata taarifa kwa njia ya sauti, ujumbe mfupi na picha kuwasaidia kuepukana na maambukizi ya Ebola katika kanda nzima.
Ili kupata taarifa kupitia kwa programu hiyo, tuma ujumbe mfupi...kupitia kwa WhatsApp kwa nambari +44 7702 348 651
WhatsApp ndio programu inayotumiwa sana kwa kutuma ujumbe mfupi barani Afrika na kwa kuitumia inaa maana kuwa ujumbe huo utawafikia mamilioni ya watu barani Afrika kupitia kwa simu zao za mkononi.
Comments
Post a Comment