BAADA YA POLISI KUMRUBUNI MWANAFUNZI WA KIKE WA MJINI MOSHI NINI KINAENDELEA?.
Ashitakiwa kijeshi.
Taarifa kutoka mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, zinaarifu kuwa jeshi la polisi nchini limemkamata na kumfikisha katika mahakama ya kijeshi askari wake Pc.Godlisen anayetuhumiwa kumtumikisha katika vitendo vya ngono mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Okaoni iliyopo wilaya ya Moshi.
Habari
zinasema kuwa, askari huyo ambaye Septemba 21 mwaka huu alimfungia
kwenye nyumba ya kulala wageni mjini moshi mwanafunzi huyo na baadaye
wawili hao kupata ajali mbaya ya pikipiki wakijaribu kutoroka, aliumia
kwenye moja ya bega lake na hivyo kushindwa kupelekwa kwenye mahakama ya
kijeshi.
Kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita, pamoja na kukiri
kuwa wameanzisha uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo, alikataa kuweka
wazi kama askari huyo amefunguliwa mashitaka ya kijeshi.
Kamanda
Koka aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, jeshi la polisi
linafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo na kwamba kama itabainika, askari
huyo atachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa.
Pamoja
na jeshi hilo kumfungulia mashitaka ya kijeshi askari huyo, taarifa
kutoka kwa mmoja wa wazazi wa mwanafunzi huyo zinadai kuwa, kuna juhudi
za makusudi zinafanywa na askari wa jeshi hilo kutaka kukwamisha
mashitaka ya kijeshi dhidi ya askari huyo.
Taarifa
zinadai kuwa, polisi wa kituo kikuu cha polisi mjini Moshi, wanajenga
ushawishi kwa wazazi wa mwanafunzi huyo kutaka kulimaliza suala hilo
kienyeji.
Mambobomba inalaani jambo hili; atua kali zitolewa kwa wafanyakazi na wanafunzi wenye tabia za kishetani kama hizi.poleni sana wazazi wa mwanafunzi husika ni kwa kiasi gani mmepambana mpaka mtoto wenu kufikia leo.
Comments
Post a Comment