T.I NDANI YA TANZANIA.


“Kwa upande wetu, tumefurahi kuleta bidhaa zetu katika bara la Afrika haswa hapa nchini Tanzania, tunadhani hili ni soko kubwa na ambalo lipo tayari kwa bidhaa zetu. Sikuja kuzijulisha bidhaa zetu hapa Tanzania pekee bali pia kuangalia mitindo mbalimbali iliyopo hapa nchini,” alisema Geter.
Duka la Pop Up litafunguliwa kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 9 alasiri na wateja watapata nafasi ya kununua nguo halisi za Hustle Gang, Akoo na Strivers Row, wamiliki wa maduka ya kisasa ya nguo boutique pia wataona bidhaa kwa ukaribu na kutoa oda zao na mashabiki watanunua na tiketi za Serengeti Fiesta hapohapo.
Ziara ya Serengeti Fiesta inatambulika kama tamasha kubwa la muziki na lenye mafanikio katika ukanda wa Afrika mashariki na kati ambalo limeweza kuwavutia zaidi ya mashabiki 500,000 katika matamasha yake yaliyohusisha wanamuziki wa kimataifa kama Jay-Z, Ludacris, 50 Cent, Rick Ross na wengine wengi.
Shoo ya mwisho ya mwaka huu ya tamasha la Serengeti Fiesta itafanyika leo Jumamosi, Oktoba 18, katika Viwanja vya Leaders Club.
Comments
Post a Comment