Posts

Showing posts from August, 2014

AJALI MBAYA :BASI LA KAMPUNI YA HOOD LAPATA AJALI KATIKA ENEO LA KIKATITI LIKIWA SAFARINI KUTOKA ARUSHA KWENDA IRINGA.

Image
Basi la Hood lililopata ajali asubuhi ya leo eneo la Kikatiti, Arusha. Raia wakishuhudia ajali ya basi la Hood ilivyotokea. Na waandishi wetu Basi la Hood lililokuwa likitoka Arusha kwenda Iringa llimepata ajali asubuhi ya leo eneo la Kikatiti, Arusha. Basi hilo lilitaka kugongana uso kwa uso na lori la mizigo, ndipo katika kukwepana ikatokea ajali hiyo. Abiria wa… Basi la Hood lililopata ajali asubuhi ya leo eneo la Kikatiti, Arusha. Raia wakishuhudia ajali ya basi la Hood ilivyotokea. Na waandishi wetu Basi la Hood lililokuwa likitoka Arusha kwenda Iringa llimepata ajali asubuhi ya leo eneo la Kikatiti, Arusha. Basi hilo lilitaka kugongana uso kwa uso na lori la mizigo, ndipo katika kukwepana ikatokea ajali hiyo. Abiria wa basi wamenusurika , ila lori lilidumbukia darajani na hakukuwa na mtu aliyepoteza maisha.

HAYA NDIYO MABAKI YA MJUSI' WA TANZANIA AMBAYE MABAKI YAKE YALITOROSHEWA UJERUMANI

Image
Haya ndo mabaki ya Mjusi kama yanavyoonekana Hii ndo sehemu ambako mabaki hayo yalipatikana UKIACHANA na Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro na hata madini ya Tanzanite, je, wajua kuwa Tanzania ina utajiri ambao ungekuwa kivutio kingine kwa watalaa nchini. Kivutio hicho kama kingekuwa hapa nchini ni mabaki ya wanyama aina ya mijusi wakubwa wa walioishi mamilioni ya miaka iliyopita (waitwao dinosaurs) hapa nchini  ambaye alichukuliwa na kupelekwa na wakoloni huko Ujerumani?                                                  Sehemu ambako mabaki hayo yamehifadhiwa Mabaki hayo  mjusi yalipatikana mwaka 1912 na kusafirishwa kwenda kuhifadhiwa Ujerumani  enzi  zile za ukoloni.  Hivi leo serikali ya Tanzania inafanya mi...

EBOLA KATIKA MUONEKANO MPYA NCHINI CONGO.

Image
sura ya kirusi kipya cha Ebola  Mto Ebola ni mto unaotiririsha maji yake kupitia katika misitu ya Congo katika jimbo la  Equateur upande wa kaskazini mwa DRC .Kirusi cha Ebola kiligunduliwa na Mbeligiji mwaka 1976 na kukipa jina la EBOLA.  Mpaka kufikia hivi sasa zaidi ya watu 1500 wamefariki kwa ugonjwa wa Ebola. japo si kwamba virusi vyote vinaua banadamu bali kuna vile vinavyoua wanyama kama nyani. nchi za Liberia, Sierra Leone, Guinea na Nigeria ndiyo nchi zilizoathiriwa zaidi na jangwa hila duniani. Uchunguzi wa kisayansi unaonesha kuwa kirusi kilicho kuwako Afrika ya kati ni tofauti na kile kilichoonekana Afrika ya kaskazini. Tafiti zaidi zinaendelea kulingana na kirusi hicho.

MATAIFA YA ULAYA NA MAREKANI YALAANI VITA NCHINI LIBYA.

Image
Mataifa ya magharibi yalaani kuenea kwa vita nchini Libya Maafisa nchini Marekani wanasema Misri na umoja wa falme za kiarabu zilihusika na mashambulio nchini Libya katika wiki iliyopita kuwalenga wanamgambo wa kiislamu wanaokabiliana na vikosi vya serikali. Afisa mmoja mkuu wa Marekani ameiambia BBC kwamba Marekani haikushirikishwa katika mashambulio hayo na ilishangazwa. Misiri imekana tuhuma hizo na hapajakuwa na tamko lolote kutoka kwa Umoja wa falme za kiarabu.Makombora hayo yaliofyetuliwa Tripoli yanasemekana kutekelezwa na Umoja wa milki za kiarabu kwa kutumia kambi za kijeshi nchini Misri. Marekani na washirika wake wanne wa Ulaya zimeshutumu wanachokitaja kama usumbufu wa kutoka nje nchini Libya. Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uingereza na Marekani zimelaani vikali mpigano na ghasia nchini Libya. Wapiganaji wa makundi mawili hasimu ndio wanaoendesha mashambulizi hayo Zimelaani pia kuongezeka kwa mapigano na ghasia ndani na kuzunguka miji ya ...

MWAROBAINI WA NDOA HUU HAPA.

Image
Wapenzi wasomaji wa Jitambue Kwanza, hakuna asiyependa kufurahia utamu wa ndoa katika maisha yake yote ya ndoa. Leo ninakukumbusha tu baadhi ya vitu vitakavyokufanya uishi katika ndoa yenye furaha na upendo siku zote. 1. SIRI -  Ukiwa katika ndoa, siri ni kitu muhimu sana ambacho huenda ukikifuata kitakuepusha na mambo mbali mbali yatakayosababisha ndoa yako iteteleke. Chagua watu maalumu unaowaamini ili uwatumie katika kuomba ushauri kwamfano, wataalamu wa mambo ya ndoa au saikolojia, ndugu wa karibu au rafiki yako wa karibu sana, na wale wote unaowaamini. Ukifanya hivyo utawaepuka wale wote wenye nia mbaya na ndoa yenu. 2. KUWA MUWAZI KWA MWENZIO  - Binadamu tumeumbwa tofauti tofauti, huenda kitabia pia tukawa hatujakamilika kuweza kumudu hali tofauti tofauti zinazotukabili katika maisha yetu, lakini yote hayo mwisho wa matatizo ni kuwa muwazi, kwani wahenga walisema; mficha maradhi kifo humuumbua. Mweleze mwenzi wako pale alipokosea ili ajirekebishe, kuliko ku...

RAIS KIKWETE BADO NI KIPENZI CHA WANA VYUO MOROGORO-MZUMBE.

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe mjini Morogoro baada ya kuwahutubia chuoni hapo Agosti 25, 2014. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika Chuo Kikuuu cha Mzumbe Morogoro baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya picha yake ya kuchorwa wakati alipotembelea Chuo Kikuu cha mzumbe ambapo walihutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho baada ya kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014. Meza kuu ikifurahia jambo wakati Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero Mhe Amos Makalla akipohutubia wanafunzi, wahadhiri na wananchi katika chuo hicho wakati Rais Kikwete alipotembelea na kuzindua ukumbi wa mihadhara na jengo la wahadhiri chuoni hapo Agosti 25, 2014. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea risala toka kwa Ra...

BAADA YA MSICHANA KUMTUPA MTOTO UVUNGUNI ,UZINDUZI KAMPENI ZA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI WAFANYIKA DAR‏

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe akizungumza katika uzinduzi wa kampeni maalumu za kitaifa za kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), zitakazo endeshwa Mkoani Mara. Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka (kwanza kulia) akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni maalumu za kitaifa za kupinga ndoa za utotoni (National Ending Child Marriage Campaign), zitakazo endeshwa Mkoani Mara. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR), Bi. Joyce Mendez Kole. Mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi nchini (UNHCR), Bi. Joyce Mendez Kole akizungumza katika hafla hiyo. Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Dk. Natalia Kanem. Mwakilishi Mkazi wa UN Women nchini Tanzania, Anna Collins (wa kwanza kushoto) akizungumza katika hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UN Women nchini Tanzania, Anna Collins, Meneja wa Haki za ...

RAIS JK KIKWETE AKIZINDUA BARABARA YA KUTOKA DUMILA KWENDA RUDEWA.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami. Sehemu ya barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami. Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Ujenzi ambao walikuwa wakisubiri tukio la ufunguzi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu w...

Shujaa wa Ebola duniani ni nani na anatokea nchi gani?pata jibu ni nani aliyetajwa kuwa shujaa wa Ebola na kwanini?

Image
Wiliam Pooley Shujaa wa Ebola duniani ni nani na anatokea nchi gani?pata jibu ni nani aliyetajwa kuwa shujaa wa Ebola na kwanini?. William Pooley anayetibiwa mjini London, baada ya kupata maambukizo ya Ebola,anatunzwa vizuri Familia ya muuguzi huyo wa kujitolea, aliyesafirishwa mjini London, baada ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, wamesema amekuwa akipata matunzo yaliyo bora. Willliam Pooley mwenye umri wa miaka 29 alirudi nchini Uingereza siku ya Jumapili na amewekwa kwenye kitengo maalumu katika hospitali ya Royal Free. Bwana Pooley ambaye alikuwa amejitolea kuwahudumia wagonjwa wa mlipuko wa Ebola barani Afrika ambao umeuwa watu 1,500 ametajwa kama shujaa na taasisi moja ya hisani inayojulikana kama Shepherd Hospice aliyoifanyia kazi nchini Sierra Leone kwa vile alijua hatari zilizokuwepo lakini akaamua kusaidia. Bwana Pooley anayetoka karibu na mji wa Woodbridge, katika kaunti ya Suffolk ni Mwingireza wa kwanza kupatikana n...