WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA TANZANIA ASHAURI BUNGE LA KATIBA LIHAIRISHWE.
Waziri
mkuu wa zamani nchini Tanzania Fredrick Sumaye amependekeza kusitishwa
kwa mjadala wa katiba mpya unaoendelea mjini Dodoma kwa kuwa inaonekana
dhahiri kuwa si muda muafaka wa kupata katiba mpya kwa sasa.
Amesema
kusitishwa kwa mjadala huo kutatoa fursa kwa watanzania kujipa muda
zaidi wa kutafakari ili kufanikisha upatikanaji wa katiba muafaka kwa
wakati unaofaa.
Kauli
hiyo ya waziri mkuu wa zamani imekuja wakati bunge hilo linaendelea na
vikao vyake mjini Dodoma vinavyohudhuriwa na wajumbe wengi kutoka chama
cha Mapinduzi CCM.
Wakati
huo huo Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), umesema Rais Kikwete ndiye
anayeweza kulitolea ufafanuzi suala la kusitisha Bunge Maalum la Katiba
na siyo mtu mwingine.
Umoja
huo pia umeendelea na msimamo wa kumtaka Rais kuwasiliana na Mwenyekiti
wa Bunge hilo, Samuel Sitta kulisitisha bunge hilo.
Comments
Post a Comment