WAGONJWA WA EBOLA WAKIMBIA ZAHANATI
Kituo kilichotengwa na kuwekewa
karantini kwa sababu ya ebola, kimeshambuliwa na zana kuporwa katika mji
mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa
kama wana dalili za ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa
Jumamosi usiku..Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Wakuu wa Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.
Comments
Post a Comment