Amwagiwa Mafuta ya Moto Usoni kisa mume.
Mwanadada
aliyefahamika kwa jina moja la Mbuva, mkazi wa Gongo la Mboto jijini
Dar, hivi karibuni amejikuta akiharibiwa uso wake kwa kumwagiwa mafuta
ya moto na shosti wake aitwaye Mama Sofia, kisa kikidaiwa ni mume wa
mtu.
Tukio
hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo inadaiwa mama Sofia
alimfanyia mwenzake unyama huo akimtuhumu kutembea na bwana
wake.Akisimulia ilivyokuwa, Mbuva alisema:
“Mama Sofia alipewa maneno ya uongo kwamba akiwa safarini eti nilitembea na bwana yake.
“Mama Sofia alipewa maneno ya uongo kwamba akiwa safarini eti nilitembea na bwana yake.
“Siku
ya tukio alinipigia simu akaniita kwake, nilikuwa sipajui ila
akanielekeza, ile nafika tu majirani zake wakamwambia mimi ndiye
nilikuwa nakwenda kulala pale na mume wake.
“Nikajaribu kujitetea lakini hakunielewa. Nikaondoka, baadaye akaniita tena, kufika pale nikakuta ugomvi kati ya mama Sofia na mumewe, ghafla mama Sofia akatoka akiwa na kikombe cha mafuta ya moto akanimwagia usoni.
“Nikaanza
kupiga kelele, watu wakajaa ndipo tukachukuliwa wote na kupelekwa
katika Kituo cha Polisi cha Mazizini na tukaandikisha, mimi nikakimbizwa
hospitali. Ameniharibu uso wangu bila kosa, Mungu atanilipia kwani
naamini malipo ni hapahapa duniani.”
Mama Sofia hakuweza kupatikama mara moja kuzungumzia tukio hilo.
Comments
Post a Comment