Mjerumani mwenye kushikilia rekodi ya dunia kwa kujitoboa mara nyingi aofiwa kuwa mchawi na kukatazwa kuingia Dubai.

 Uso wake Rolf Bushholz ulivyo na maumbile kama pembe
Mwanaume mmoja kutoka Ujerumani 
anayeshikilia rekodi ya dunia ya kuwa mtu aliyetoboa zaidi mwili wake, 
Rolf Buchholz amekatazwa kuingia Dubai.
Rolf Buchholz, ametoboa mwili wake mara 453  ikiwemo usoni mwake na ana pembe mbili juu ya paja la uso wake.
Rolf Bushholz aliyenyimwa ruhusa ya kuingia Dubai.
Bwana Buchholz alieleza BBC kuwa maafisa wakuu katika uwanja wa ndege walihofia huenda alikuwa ni '' mchawi'' .
Mtaalamu huyu wa tarakilishi alitambulika na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness, kama mwanaume aliyetoboa mwili wake zaidi duniani mwaka wa 2012.

  Rolf Bushholz katika moja ya maonyesho yake 
Onyesho lake katika mgahawa maarufu wa Irque le Soir ulioko katika hoteli ya Fairmont Hotel Dubai lilifutiliwa mbali.

Mdomo wake uso wake Rolf Bushholz  ulivyotogwa 
Bwana Rolf amesema kuwa mizigo yake bado iko Dubai na aliapa kwenye mtandao wa kijamii kuwa hatarudi tena katika milki za Kiarabu.
Polisi na Maafisa wa usafiri wa ndege nchini Dubai hawajazungumzia swala hilo.
 
 
 
Comments
Post a Comment