NABII ASEMA EBOLA HAITOINGIA TANZANIA.


Safu hii leo inahojiana na Nabii Yasp P. Bendera  ambaye ana kanisa lake lililopo Yombo Buza Dar. Amekuwa akihudumia watu kwa miaka mitatu sasa.
Nabii Yaspi Paul Bendera akiwa katika studio za Global TV Online kabla ya mahojiano.
Anadai aliwahi kutabiri ugonjwa wa dengue…

Safu hii leo inahojiana na Nabii Yasp P. Bendera  ambaye ana kanisa lake lililopo Yombo Buza Dar. Amekuwa akihudumia watu kwa miaka mitatu sasa.
Nabii Yaspi Paul Bendera akiwa katika studio za Global TV Online kabla ya mahojiano.
Anadai aliwahi kutabiri ugonjwa wa dengue kutokea hapa nchini na akatoa dalili, ukaingia , akatabiri mafuriko yakatokea na pia alitabiri kuhusu ugonjwa wa ebola lakini akasema Tanzania haujaingia.
Alisema ebola haitaingia Tanzania ikiwa Watanzania watazingatia  masharti.
Akasema: “Tukiyafuata  masharti hautatokea, lakini tukipuuza ukaingia basi utaua mbunge mmoja na  madaktari wawili.”Akielezea historia yake nabii huyo alisema : “Baba yangu alikuwa Katekista katika Kanisa la Roma.
Nilikuwa katika dini hiyo nikawa mwenyekiti Wawata, Kanisa la Ngerengere. Baadaye nikawa naongoza kundi la watoto zaidi ya mia tatu. Nilipata ufunuo nikaingia Kanisa la Ufunuo. Nilikuwa sina mpango wa kuwa nabii. Baadaye niliambiwa moyoni kuwa niwe nabii, nikaanzisha kanisa pale nikiwa na waumini watano, sasa wapo maelfu.
Nabii Yaspi akijibu maswali ya wanahabari wa GPL (hawapo pichani), mbele ya kamera za Global TV Online.
Huduma anazozitoa ni pamoja na kuwahudumia watu wanaohitaji huduma mbalimbali na huwa anashauri watu na kuwaombea wagonjwa wote bila kujali ni dini au kabila gani na kuwatabiria. Mahojiano kati yake na wana habari wa Global pamoja na ‘kruu’ ya Global Tv Online ni haya yafuatayo:
Mwandishi: Homa ya dengue ulitabiri lini? Baada ya utabiri ukataka kuonana na Rais Jakaya Kikwete, je ulionana naye ?
Nabii: Nilitabiri mwezi wa pili mwaka huu na nilitakiwa na Mungu nionane na mheshimiwa rais nimuelezee. Kulikuwa na siri ya kumuambia isipokuwa nilitakiwa kumueleza mkuu wa nchi na siyo mtu mwingine na ndiyo inayoleta majanga nchini. Bahati mbaya sikupata nafasi ya kuonana naye na ndiyo maana mpaka sasa kuna madhara yanatokea hapa nchini.
Mwandishi: Ni siri gani hiyo?
Nabii: Hata wewe sitakuambia, ni ya rais.
Mwandishi: Umetabiria na kuwaombea wangapi?
Nabii: Niliowahi kuwaombea ni wengi, kwa kweli sikuwa narekodi lakini wengi wamepona na wengine walikuja kutoa ushuhuda. Huduma tunayotoa ni kwa dini zote na Mungu hana dini.
Mwandishi: Nitaaminije kuwa wewe siyo msanii na kwa nini unatabiri mabaya tu?
Nabii Yaspi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa GPL kutoka kulia ni Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist, Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari (IT), Clarence Mulisa na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa, Amran Kaima.
Nabii: Ninapotabiri huwa natoa taarifa baada ya Mungu kuniambia, utaamini ukija kwenye huduma yangu. Huwa natabiri hata mazuri. Wakati wa Nuhu, aliposema kuna gharika walimuona ni muongo, lakini wangekubali wasingeangamia.
Mungu anataka umuabudu na uachane na mambo mabaya, hata mimi ninapotabiri kuna watu hawaamini lakini ipo siku wataamini.
Mwandishi:  Nitaaminije kuwa wewe ni mtabiri?
Nabii: Usisikie ushuhuda, uje mwenyewe kanisani na hapo utaona kama mimi ni nabii au siyo.
Mwandishi: Unawasiliana vipi na Mungu?
Nabii: Mungu ni roho, ninapoongea na Mungu huwezi kusikia lakini ipo njia ya hata wewe kusikia, ukija kanisani nitakuonesha.
Mwandishi: Je, umeolewa?
Nabii: Nimeolewa na nina watoto wanne. Akija mtu ambaye ndoa yake ina vurugu najua nitafanya nini ili kuondoa hiyo hali.
Mwandishi: Inadaiwa uliwahi kufa na kufufuka ilikuwaje? Na kuna taarifa kuwa uliwahi kumtibu waziri mmoja, ilikuwaje?
Nabii Yaspi akiwa katika picha na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.
Nabii: Nilikuwa na tatizo la kushuka presha enzi hizo, nilikwenda hospitali ya jeshi kutibiwa, nikapoteza fahamu nikazungushiwa shuka za kijani, nikasikia sauti inaniambia hutakufa, nikafufuka, manesi wakakimbia baadaye wakaniambia kuwa nilikuwa nimekufa na madaktari walishaandika hivyo, kungekuwa na mochwari pale ningekuwa nimepelekwa.
Kuhusu waziri, dada mmoja aliniambia kuwa kuna waziri anaumwa sana. Dada huyo alinipeleka kwa waziri huyo (jina tunalo) nikamuombea na kumuambia kuwa ndani ya siku kadhaa utapona. Akapona, akaenda India kupimwa afya, alinipigia simu akiwa huko nikamtabiria kuwa atakuwa waziri kamili kwani wakati huo alikuwa naibu baada ya baraza la mawaziri kuvunjwa, akateuliwa kuwa waziri kamili kama nilivyomtabiria.
Mwandishi: Manabii wanatibu kwa vitambaa,  inakuwaje hivyo?
Nabii: Yesu alitengeneza tope akampaka kipofu akapona, kama Yesu alitengeneza tope akamponya, haishangazi manabii kutumia vitambaa au mafuta. Vitu hivyo zamani na hata chumvi ni muhimu sana. Ukweli ni kwamba mwenye maarifa ya Kimungu huweza kumpiga shetani.
Mwandishi: Kama nataka kuwa nabii, nifanyeje?  
Nabii Yaspi akipozi na Mwandishi Nyemo Chilongani wa GPL.
Mabii: Unabii hausomewi kama udaktari ni neema mtu anashushiwa kutoka kwa Mungu na hupewa yeyote. Mwandishi: Tanzania kuna utitiri wa manabii, wapo wangapi na yupi si nabii?
Nabii: Mimi kazi yangu siyo kujaji watu wengine. Siwezi kusema fulani ni nabiii na fulani siyo nabii.
Imeandikwa nabii wa kweli ni yule anenaye likatendeka. Vitabu vinasema mtangetange mtafute Neno la Mungu. Hata hivyo, nitahubiri kwa nyimbo na ndiyo maana nitazindua albamu yangu Septemba sita PTA.
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS

Comments

Popular posts from this blog

STYLE KALI:TUMIA HII NDANI YA DAKIKA MOJA TU MWANAMKE AMEKOJOA.

KISIMI (kinembe) kikichezewa mwanamke anaweza kuwataja maawara zake wote.