Ebola liberia, wanaswa waliotoroka hospitalini.
Kituo kilichotengwa na kuwekewa
kwa sababu ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Ebola, kimeshambuliwa na
zana kuporwa katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia.
Watu kama 20 hadi 30 waliowekwa hapo kuangaliwa
kama wana dalili za Ebola walitoroka baada ya kituo hicho kuporwa
Jumamosi usiku.Washambuliaji walipora magodoro na vitu vingine.
Mwandishi wa BBC katika kanda hiyo anasema pengine washambuliaji walikerwa kuwa kituo hicho kimewekwa katika mtaa wao.
Mafisa wakuu nchini Liberia wanajaribu kuwatafuta wagonjwa waliotoroka ili kuwarejesha tena kwenye kituo hicho.
Watu zaidi ya 400 wamekufa kwa sababu ya ebola nchini Liberia kati ya zaidi ya 1,000 katika kanda ya Afrika Magharibi.
Comments
Post a Comment