Watu wawili wafa kwa Ebola nchini Congo.


 25 Agosti, 2014 - Saa 08:30 GMT
Serikali ya DRC imedhibitisha Ebola imeua watu wawili kaskazini
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imesema watu wawili wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola, uliolipuka kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo.
Hao ni wagonjwa wa kwanza wa Ebola kuripotiwa nje ya Afrika Magharibi tangu kuzuka kwa ugonjwa huo huko, ingawaje haijaeleweka wazi kama vifo vya watu hao vinahusiana na mlipuko wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi.

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema kasi na kiwango cha milipuko hiyo hakijawahi kutokea hapo kabla.Mpaka sasa watu 1,427 wamekufa kutokana na maambukizo ya virusi vya Ebola.
Watu wanaokadiriwa kufikia 2,615 Afrika Magharibi wameambukizwa ugonjwa wa Ebola tangu uzuke mwezi Machi mwaka huu.

Hakuna tiba inayojulikana kutibu ugonjwa huu lakini 







Kirusi cha Ebola
baadhi ya watu walioambukizwa virusi vya Ebola 
wamepata nafuu baada ya kupewa dawa ya Zmapp iliyo katika majaribio.
Hata hivyo dawa hiyo imeadimika kwa sasa.
Pia Jumapili, mfanyakazi wa afya wa Uingereza aliambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone na kurejeshwa Uingereza akisafirishwa na ndege ya jeshi la Uingereza, RAF.
Ni mgonjwa wa kwanza Mwingereza kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya Ebola wakati wa mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo.
Marekani imetuma vifaa vya tiba kusaidia kupambana na mlipuko wa Ebola nchini Liberia.
Watu kadha wamekufa katika kipindi cha mwezi uliopita baada ya kuugua homa isiyojulikana katika jimbo la Equateur katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Jumapili, Waziri wa Afya wa DR Congo Felix Kabange Numbi amesema watu wawili kati ya wanane waliopimwa ugonjwa Ebola wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo.
Ebola ilivyoenea Afrika
Ameiambia BBC kuwa eneo la karantini litawekwa katika eneo la kipenyo cha kilomita za mraba 100 katika eneo la Boende ambao wagonjwa wamegundulika.
Amesema huu ni mlipuko wa saba wa ugonjwa wa Ebola nchini DR Congo.
Virusi vya ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kwanza viligundulika nchini humo mwaka 1976 karibu na Mto Ebola.
Bwana Numbi amesema vipimo zaidi vinafanyika.
Jumamosi, bunge la Sierra Leone lilipitisha sheria mpya kuwa ni kosa la jinai kuwaficha wagonjwa wa Ebola.

Comments

Popular posts from this blog

STYLE KALI:TUMIA HII NDANI YA DAKIKA MOJA TU MWANAMKE AMEKOJOA.

KISIMI (kinembe) kikichezewa mwanamke anaweza kuwataja maawara zake wote.