MWANDISHI WA HABARI AKATWA KICHWA.
Mwandishi wa habari wa Marekani aliyekatwa kichwa, James Wright Foley (kushoto), akiwa amevishwa kanzu maalum.
Kabla
ya kuuawa kwake, Foley, aliwataka marafiki, wanafamilia wake na wapenzi
wake wote kupambana na “wauaji wangu wa kweli” ambao ni serikali ya
Marekani.
Foley
akiwa na muuaji wake ambaye alisema kitendo cha kumwadhibu mwandishi
huyo ni kulipiza kisasi mashambulizi ya ndege za Marekani nchini Iraq.
Foley enzi za uhai wake hadi alipopotea Novemba 2012, baada ya kutekwa huko Taftanaz, kaskazini mwa Syria.
Mama yake Foley, Diana, na baba yake John, wakiwa katika mkesha kanisani kuwataka wapiganaji wa ISIS kuwaachia mateka wao.Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo, serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwa nini James Foley auawe.

Comments
Post a Comment