MSANII MKONGWE WA SWAHILIWOOD JOHARI ANAMCHUKIA MSANII IRINE UWOYA SABABU NI ...SOMA HII.
Msanii 
 Johari Blandina ‘Chagula’ ambaye ni star mkongwe Swahiliwood amesema 
kuwa anamshukuru Mungu kwa kuutunza muonekano wake na kuwa kama kijana 
licha ya umri wake kuwa mkubwa tofauti na baadhi ya waigizaji wenzake wa
 kike ambao hujiachia na kuonekana wazee licha ya umri wao kuwa mdogo.
Akizungumza na Filamucentral Johari alisema:
“Wasanii
 wa kike wengi ni watoto wadogo lakini kwa sababu ya kujiachia 
wanaonekana kama watu wazima lakini ukweli ni watoto wadogo sana, 
namshukru Mungu nimeanza sanaa kitambo lakini mwili wangu upo fiti,”
Johari
 alimtolea mfano Irene Uwoya ambaye ni shoga’ke wa karibu kuwa 
anaonekana mkubwa kwasasa sababu ya kujiachia licha ya kwamba amempita 
miaka kadhaa. 
Vile
 vile Johari amesema kuwa kawasasa amerudi kwa moto wa kasi kama 
muigizaji kama awali baada ya kuwa upande wa producer kuwapa nafasi 
chipukizi ambao wengi amesema wameshindwa, hivyo amerudi mwenyewe kwenye
 game.

 
 
 
Comments
Post a Comment