TUNDAMAN ASHAURIWA KUGOMBEA URAISI NA MZEE MKUBWA MH.E.LOWASA.
Tundaman: Iddi Azan ananiandaa kuwa Mbunge, ‘napata ushauri kwa mheshimiwa Lowasa..’
Tundaman ameweka wazi mpango wa kuingia rasmi katika siasa na kukitafuta kiti cha ubunge katika uchaguzi mkuu baada ya 2015.
Akiongea na Times Fm, Tundaman ameeleza kuwa alipata moyo na wazo la kugombea kiti cha ubunge kutoka kwa mbunge wa Kinondoni, mheshimiwa Iddi Azan.
“Rafiki yangu sana Iddi Azan, sometimes nikikaa nae sehemu wananchi wananishangilia mimi anasema ‘Tunda unapendwa hivi, basi na wewe uje kugombania mambo haya’. Nikasema basi sawa na hilo suala nalifanyia kazi, kwa hiyo mimi ntachukua details nyingi kutoka kwake na yeye ndiye anaeniandaa mimi kuwa mbunge baadae (sio 2015).”Amesema Tunda Man.
Ameeleza pia kuhusu jinsi anavyopata ushauri wa siasa kutoka kwa wanasiasa wakubwa akiwemo waziri mkuu wa zamani Mheshimiwa Edward Lowasa.
“Kwa sababu niko karibu sana na waheshimiwa wananishauri, kwa hiyo najua nini cha kufanya na nini nisifanye. Sometimes nakaa na Lowasa ananiambia vitu vingi mheshimiwa kwamba siasa iko hivi… kwa hiyo kuna vitu fulani mimi ninapata bila wao kujua napata kutoka kwao. Lengo baadae nitakapovifanya nisiwe nakosea, niwe straight katika kuvifanya ili nifanikiwe.”
Comments
Post a Comment