KIGOMA NA ARUSHA HALI YA HATARI KWA MWAKA 2014.
Watu watatu wamekufa akiwepo mtoto mchanga na wengine sita kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria (Hiace) kurushiwa bomu na watu wasiojulikana huko Kasesema, Kigoma alfajiri ya leo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Buhigwe (OCD), Samwel Utonga alisema basi hilo lilikuwa likotokea Kilelema kwenda Kasulu Mjini ambapo watu hao walilirushia kitu kinachoaminika kuwa ni bomu.
Kamanda Utonga amesema majeruhi hao wamehamishiwa Hospitali ya Kasulu toka Hospitali ya Muyama baada ya hali zao kuwa mbaya.
Comments
Post a Comment