DIAMOND MSANII MAARUFU WA BONGO FLEVA AFUATILIWA KUHUSIANA NA MADAWA YA KULEVYA.

NIkweli kimenuka! Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ yupo kikaangoni, habari zinadai kwamba kila anaponyanyua miguu, kikosi chakupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini chini ya kamishna wake,
Godfrey Nzowa nao wananyanyua miguu yao kumfuatilia, Amani limesheheni.
Mbongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi.
Habari za kiintelijensia zilidai kwamba, kisa cha kikosi hicho kufanya hivyo kinadaiwa kuwa, serikali inamhofia kujihusisha na biashara hiyo haramu ya kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’ nje ya nchi kwa kutumia kivuli cha kwenda kufanya shoo.
Akizungumza na wanahabari wetu jijini Dar, Jumatatu iliyopita, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa kitengo hicho ambaye hakupenda kuchorwa jina gazetini, alisema Diamond amepewa maelekezo yote muhimu.
MAELEKEZO ALIYOPEWA
“Tumempa maelekezo Diamond, atuletee mikataba ya shoo zote anazokwenda kuzifanya nje ya nchi ili tujiridhishe kama kweli ni halali au anakwenda kwa ajili ya biashara nyingine.
“Hiyo yote inatokana na uchunguzi wetu kwake kuhusu akaunti zake za benki kuonesha kwamba ana fedha nyingi sana zinazotia shaka kama amezipata kihalali,” alisema afisa huyo.
‘Diamond Platnumz’ akiwa kazini.
KUNUNUA NYUMBA
Afisa huyo aliendelea kusema kwamba, uchunguzi wao pia umebaini kwamba, msanii huyo wa Bongo amekuwa akinunua nyumba kila anaporejea kutoka kwenye shoo zake nje ya nchi, jambo ambalo taasisi haiamini kama kweli analipwa pesa nyingi kwa shoo moja, kiasi cha kumwezesha kununua nyumba jijini Dar.
“Tumebaini kwamba Diamond kila akirudi nchini kutoka kwenye shoo zake hununua nyumba. Analipwa kiasi gani cha fedha kule kwenye shoo? Hapa ndipo tunaposimamia sisi,” alisema afisa huyo huku akigongea msumari kuwa Diamond mwenyewe amekatazwa kuzungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu kutakiwa kuwasilisha mikataba ya shoo zake za nje.
 KUNA UKWELI?
Amani lilifuatilia na kubaini kwamba, Diamond aliporejea kutoka kwenye safari yake ya Marekani hivi karibuni, alinunua nyumba kwa Sh. milioni 80 iliyopo maeneo ya Mwananyamala-Magengeni, Dar.
Siku za nyuma, msanii huyo aliwahi kuripotiwa kununua nyumba zaidi ya mbili maeneo ya Kijitonyama, Dar, kiasi cha kuandikwa na vyombo vya habari kwamba amenunua mtaa.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa.
KUHUSU AKAUNTI YA BENKI
Diamond mwenyewe aliwahi kuhojiwa katika Kipindi cha Take-One kinachorushwa hewani na CloudsTV ambapo alipoulizwa akaunti yake inasomaje, alijibu kuwa ina zaidi ya bilioni moja hivi.
DONDOO ZA UWEZO WA DIAMOND
1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.
2. Yupo kwenye mazungumzo na promota wa Rwanda kufanya shoo moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 (zaidi ya Sh. milioni 190).
3. Malipo ambayo hupokea kwa shoo zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000 (zaidi ya Sh. milioni 40).
4. Tangu mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya Sh. milioni 100.
5. Anamiliki nyumba kadhaa
 jijini Dar ambazo amepangisha watu.
6. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake, Papa Misifa ilibidi amlipe Sh. milioni 18.
NZOWA AZUNGUMZA NA AMANI
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Nzowa ambapo alipopatikana na kuulizwa, alisema:
Sehemu ya madawa ya kulevya yaliyowahi kukamatwa.
“Ni kweli! Sisi kila mtu mwenye kipato cha kutia shaka lazima tumchunguze. Diamond kama ana mali zote kwa nini tusimchunguze. Ikithibitika anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ama zake ama zetu huo ndiyo utaratibu wetu.”
DIAMOND SASA
Amani lilimsaka Diamond na kumuuliza kama analijua kasheshe hilo ambapo alisema:
“Najua, ila nimegundua kuna watu wamepanga kunishusha chini kisanii ndiyo wanaoeneza taarifa kwamba mimi nasafirisha unga.”
Amani: Sasa unadhani kwa nini hao watu unaosema wamependa kukushusha kisanii wasitumie njia nyingine, hasa ya sanaa wakatumia hiyo ambayo unasema si kweli?
Diamond: We elewe hivyo kaka (akakata simu).
SAFARI ZA NJE
Kwa kipindi kirefu sasa Diamond ambaye ni mpenzi wa Wema Isaac Sepetu, amekuwa akisafiri nchi mbalimbali kwa shoo na mambo binafsi ambapo mbali na nchi kibao za Bara la Afrika, ameshasafiri nchi nyingi zikiwemo Marekani, Uingereza, China, Norway, Ujerumani, Dubai na nyinginezo.  

Comments

Popular posts from this blog

STYLE KALI:TUMIA HII NDANI YA DAKIKA MOJA TU MWANAMKE AMEKOJOA.

KISIMI (kinembe) kikichezewa mwanamke anaweza kuwataja maawara zake wote.